24 Juni 2020 - 12:55
Rais Rouhani: Jamhuri ya Kiislamu inawaenzi wanawake

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema moja ya fahari za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kuwa inawaruhusu wanawake waendeleze harakati zao katika sekta mbali mbali.

Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Akizungumza Jumatano katika kikao cha baraza la mawaziri, Rais Rouhani ametuma salamu za pongezi kwa mnasaba wa 'Siku ya Kitaifa ya Msichana' nchini Iran na kuongeza kuwa Uislamu hauwabagui wanawake.

Amesema baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, mazingira mazuri yaliibuka ili kuwawezesha wanawake kujishughulisha katika sekta za sayansi, utafiti na uzalishaji. Aidha amesema leo wasichana wa Iran wamejaa katika vyuo vikuu na wanaohitimu wanafanya kazi katika mahospitali, viwanda, idara za serikali na kadhalika. 

Kwingineko katika hotuba yake, Rais Rouhani ameashiria matatizo yaliyoko katika jamii na kusema ni jukumu la serikali kuyatatua.

Ameongeza kuwa, matatizo yaliyoko hivi sasa yanatokana na janga la COVID-19 ambalo liliibuka miezi michache iliyopita na pia vikwazo vya kidhalimu vya Marekani. Amesema Iran imekuwa ikikabiliwa na vikwazo shadidi kwa muda wa miaka mitatu sasa na kuongeza kuwa maafisa wa serikali wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kuwa matatizo yanatatuliwa.

342/